Diodi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Diodi mbalimbali

Diodi ni kijenzi au kiambajengo elektroniki muhimu. Inafanya kazi kama valvu ya umeme ikiruhusu mkondo wa umeme kutiririka kuelekea upande mmoja tu.

Diodi hutumiwa kubadilisha mkondo geu (AC) kuwa mkondo mnyovu (DC). Zinapatikana mara nyingi katika mitambo ya kutolea umeme kama vile ugawi wa umeme wa kompyuta. Kwa ndani vijenzi vya kompyuta hutumia mkondo mnyofu lakini umeme kutoka nje ni mkondo geu unaohitaji kubadilishwa, kazi inayofanya na diodo katika ugawi wa umeme.[1][2][3]]]

Siku hizi diodi hutumiwa zaidi na zaidi kwa umbo la diodi itoayo nuru (LED) ambazo siku hizi zinatumiwa katika taa kwa matumizi kidogo cha nishati kuliko taa za kawaida.

Siku hizi diodi hutengenezwa kwa kutumia dutu za nusu kipitishi (ing. semiconductor) kama vile silikoni au germani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tooley, Mike (2013). Electronic Circuits: Fundamentals and Applications, 3rd Ed.. Routledge, 81. ISBN 978-1-136-40731-4. 
  2. Crecraft, Filip Mincic (2002). Analog Electronics: Circuits, Systems and Signal Processing. Butterworth-Heinemann, 110. ISBN 0-7506-5095-8. 
  3. Horowitz, Paul (1989). The Art of Electronics, 2nd Ed.. London: Cambridge University Press, 44. ISBN 0-521-37095-7.