Desoksimetasoni
Desoksimetasoni (Desoximetasone), inayouzwa kwa idadi ya majina ya chapa mbalimbali, ni dawa inayotumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ngozi uitwao dermatitisi na psoriasisi.[1] Inatumika kwa ngozi, mara mbili kwa siku.[1]
Madhara yake ya kawaida yanajumuisha kuungua, kuongezeka kwa ukuaji wa nywele, kuharibika kwa ngozi, chunusi, maambukizi, kudhoofika kwa ngozi, na alama ya kunyoosha (striae).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa unaotokea mwili unapotengeneza homoni ya cortisol nyingi (Cushing's syndrome).[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Ni katika dawa za kuzuia mwasho (corticosteroids).[1]
Desoksimetasoni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1977[1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[2] Nchini Marekani, mrija wa gramu 60 unagharimu takriban dola 35 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Desoximetasone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "Desoximetasone Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Desoksimetasoni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |