De Standaard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
De Standaard
Jina la gazeti De Standaard
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1918
Eneo la kuchapishwa Ubelgiji
Nchi Ubelgiji
Mhariri Bart Sturtewagen
Mmiliki Corelio
Makao Makuu ya kampuni Gossetlaan 28
Groot-Bijgaarden B-1702
Nakala zinazosambazwa * 1999: 98,169
* 2000: 98,235
* 2001: 95,867
* 2002: 93,500
* 2003: 94,890
* 2005: 97,226 (Agosti)
Tovuti http://www.standaard.be/

De Standaard ni gazeti la kila siku la Kiflemish linalochapishwa nchini Ubelgiji na Corelio (hapo zamani lilijulikana kama VUM). Usambazaji wake ulikuwa nakala 97,226 katika mwaka wa 2005. Hapo jadi, lilikuwa jarida la Kikristo na Kidemokrasia , likihusishwa na Chama cha Flemish cha Kikristo-kidemokrasia, na lilikuwa gazeti pinzani kwa gazeti la De Morgen. De Morgen lilikuwa gazeti la kila siku la Chama cha Socialist Flemish. Hata hivyo, hivi leo, gazeti hili halipendelei msimamo wowote wa kisiasa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 1911, Frans Van Cauwelaert alianzisha Ons Volk Ontwaakt, jarida la kuchapishwa kila wiki na shirika la wanafunzi wakatoliki wa Flemish.

Katika mwaka wa 1914, Van Cauwelaert, Alfons Van de Perre, na Arnold Hendrix waliunda kampuni ya uchapishaji, De Standaard N.V (Kundi la Standard). Lengo lao lilikuwa kuchapisha gazeti la Katoliki, la kihafidhina na la kila siku jijini Brussels, na liitwe De Standaard. Kaulimbiu ya De Standaard ilikuwa Alles voor Vlaanderen - Vlaanderen voor Kristus("Kila kitu kwa Flanders - Flanders kwa Kristo) ikafupishwa kuwa AW-WK. AW-WK ilichapishwa katika ukurasa wa kwanza wa De Standaard hadi mwaka wa 1999.Toleo la kwanza lilichapishwa mnamo 22 Novemba 1914, lakini uchapishaji ukaachishwa kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. De Standaard halikuchapishwa tena mpaka 4 Desemba 1918, baada ya vita kuisha.Gustave Sap, ambaye alijiunga na bodi ya wakurugenzi katika mwaka wa 1919, ndiye aliyetoa pesa zilizohitajika kwa upanuzi wa De Standaard wa awali.

Katika mwaka wa 1940, katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia,Wajerumani wa Nazi walidhibiti Ubelgiji. Uchapishaji wa De Standaard ukasimamishwa. Hata hivyo, gazeti jipya ,Het Algemeen Nieuws,(Habari kwa Jumla) lilianza kuchapishwa na wafanyikazi na vifaa vya De Standaard huku wakichapisha habari iliyokubaliwa na serikali ya Nazi.Baada ya ukombozi wa Ubelgiji katika mwaka wa 1944, usimamizi wa Kundi la Standard ulishtakiwa kwa kushirikiana na wavamizi wa Nazi na kampuni hii ikapigwa marufuku kwa miaka miwili. Kampuni mpya ikaanzishwa ; De Gids N.V. ambayo ikaanza kuchapisha gazeti jipya la De Nieuwe Standaard katika mwezi wa Novemba 1944.Magazeti mengine ya hapo awali yaliendeleshwa na De Gids.

Katika mwaka wa 1947, kupigwa marufuku kwa Kundi la Standard kuliondolewa na kwa ruhusa ya mahakama ilianza kuchapisha magazeti yake tena. De Nieuwe Standaard likaitwa De Nieuwe Gidsna kisha , tangu 1 Mei, likapewa jina la De Standaard tena.

Katika miaka ya 1960 na miaka ya 1970, gazeti la De Standaard lilikuwa maarufu kwa makala yake yaliyowasilisha habari bora sana kuhusu masuala ya kigeni. Kwa mfano, licha ya uhusiano wake wa Katoliki na wa uhafidhina, De Standaard lilishutumu sera za Marekani za kutekelezwa katika Kusini mashariki mwa bara la Asia.

Hata hivyo, hali ya kifedha ya Kundi la Standard ilidhoofika sana , kampuni hii ikapata shida zaidi katika mwaka wa 1976. Kundi la Standard likatangaza kuwa limedhibitiwa na shida hizo za kifedha mnamo 22 Juni wa mwaka huo. De Standaard liliokolewa na André Leysen, mfanyibiashara wa Ubelgiji, aliyeanzisha Vlaamse Uitgeversmaatschappij N.V. (VUM - "Ushirikiano wa Wachapishaji wa Flemish"). VUM ilichukua magazeti yote ya Kundi la Standard, na likawa kampuni linalochapisha De Standaard. VUM ilibadilisha jina lake kuwa Corelio katika mwaka wa 2006.

Katika mwaka wa 2004, De Standaard likabadilisha kutoka mtindo mpana wa uchapishaji hadi mtindo mdogo zaidi.

Waandishi Maarufu[hariri | hariri chanzo]

 • Gaston Durnez
 • Maria Rosseels (1916-2005), mkosoaji wa filamu na mwandishi.
 • Mia Doornaert, mhariri wa kidiplomasia

Usambazaji wa nakala[hariri | hariri chanzo]

 • 1999: 98,169
 • 2000: 98,235
 • 2001: 95,867
 • 2002: 93,500
 • 2003: 94,890
 • 2005: 97,226 (Agosti)

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

 1. Wasifu wa Kampuni Archived 26 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
 2. http://www.pressdisplay.com/pressdisplay/viewer.aspx?cid=3214

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]