Nenda kwa yaliyomo

Daytime Friends

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daytime Friends
Daytime Friends Cover
{{{Type}}} ya Kenny Rogers
Aina studio
Urefu 36:33
Lebo United Artists Records
Wendo wa albamu za Kenny Rogers
Kenny Rogers
(1977)
Daytime Friends
(1977)


Daytime Friends ni jina la albamu ya tatu ya [Kenny Rogers]]' ambapo albamu hii ilitengenezwa katika studio ya United Artists Records, iliyotoka dunia nzima mwaka 1977. ilikuwa ni albamu yake ya pili katika mafanikio kufuatia ile ya mwaka 1976. (Albamu yake ya kwanza iliyoitwa Love Lifted Me ilipata mafanikio ya wastani na albamu yake yenye jina lake mwenyewe Kenny Rogers ndiyo iliyofanikiwa kufika namba moja ya katika chati ya muziki wa kantri ya Marekani na kufanikiwa pia kufanya vizuri katika nchi mbalimbali

Kuhusu Albamu

[hariri | hariri chanzo]

Albamu hii ilitoa nyimbo 10 bora ambazo zilifika katika nafasi ya kwanza katika chati ya nyimbo za na wimbo wa "Sweet Music Man" ambao aliutengeza mwenyewe ukifika katika nafasi ya #9. Wimbo wa "Sweet Music Man" baadae ulikuja kuimbwa na wanamuziki wengine kama vile Dolly Parton. Wimbo mwingine wa "Am I Too Late?", ambao pia upo katika albamu hii ambao Kenny mwenyewe anasema wimbo huo ni moja kati ya nyimbo anazozipenda

Albamu hii inahusiana na hadithi mbalimbali kitu ambacho kimemfanya Kenny Rogers kuwa maarufu. Katika wimbo wa I'll Just Write My Music and Sing My Songs" ikiashiria mwanamuziki ambaye ana mafanikio na anaishi maisha mazuri lakini hana furaha wala mapenzi katika maisha. Pia kuna nyimb mbalimbali za mapenzi zinahusu mafanikio mbalimbali furaha na mahusiano kama vile "My World Begins and Ends With You" na nyingine zikiwa zinahusu masuala uamnifu na kusema ukweli kama vile "Lying Again"

Nafasi mbalimbali

[hariri | hariri chanzo]

Albamu hii ilifika nafasi ya #2 katika chati ya muziki ya kantri na pia ulikuwa wimbo wa bora wa pop, lakini aliendelea kusindikizwa na nyimbo zilizotangulia na zilizokuwa na mafanikio zaidi, hususani katika albamu ya Kenny Rogers na kutoka kwa kifurushi cha Kenny Rogers cha Ten Years Of Gold. Hata hivyo albamu hii ilifanya vizuri pamoja na zile albamu tatu ambazo zote zilifakiwa kufika katika nafasi ya tatu katika chati ya Billboard katika nyimbo zalizoongoza kwa mauzo katika wiki moja, rekodi ambayo bado haijafikiwa hadi sasa. Mwaka 2007, miaka 30 baada ya kutoka kwa albamu hiyo, albamu hii iliweza kupatikana kwa njia ya wavuti kwa mara ya kwanza.

Wimbo unaobeba jinala albamu hii, wakati mwingine ikiitwa "Daytime Friends (Night-time Lovers)" wimbo huu umesharudiwa mara na wanamuziki mbambali kama vile kundi la nchini Ireland la Westlife.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]
  1. Daytime Friends [3:10]
  2. Desperado [3:44]
  3. Rock And Roll Man [2:46]
  4. Lying Again [2:41]
  5. I'lL Just Write My Music And Sing My Songs [2:55]
  6. My World Begins And Ends With You [2:43]
  7. Sweet Music Man [4:16]
  8. Am I Too Late [3:31]
  9. We Don't Make Love Anymore [3:51]
  10. Ghost Of Another Man [2:57]
  11. Let Me Sing For You [4:39]