Nenda kwa yaliyomo

David Bader (mtalaamu wa tarakilishi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

David A. Bader (amezaliwa Mei 4, 1969) ni Profesa na mkurugenzi wa taasisi ya takwimu za kisayansi katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha New Jersey[1]. Kabla alitumikia kama mwenyekiti wa idara ya sayansi ya kompyuta katika uhandisi kwenye Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Georgia.

Mwaka 2007 alipewa nafasi ya mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kichakato kipya cha makampuni ya Sony na Toshiba kwenye chuo hicho[2].

Mwaka 2021 alipokea tuzo kwa mafanikio yake ya kubuni kompyutasupa kwa ajili ya mfumo ya Linux aliychowahi kuunda 1998 akiwa kwenye Chuo Kikuu cha New Mexico akitumia vipuli vya kawaida vilivyopatkana madukani.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "NJIT to Establish New Institute for Data Science". NJIT News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-09.
  2. "Wayback Machine" (PDF). web.archive.org. 2007-11-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-11-29. Iliwekwa mnamo 2022-09-09.
  3. "David Bader to Receive 2021 IEEE CS Sidney Fernbach Award |" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-09.