Dambisa Moyo
Dambisa Felicia Moyo, Baroness Moyo (alizaliwa 2 Februari 1969) ni mchumi na mwandishi kutoka nchini Zambia, maarufu kwa uchambuzi wake wa uchumi mkuu na masuala ya kimataifa. Ameandikavitabu vitano juu ya masuala ya kiuchumi. Ikiwa ni pamoja Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa (2009), How the West Was Lost: Fifty Years of Economic Folly – And the Stark Choices that Lie Ahead (2011), Winner Take All: China's Race for Resources and What It Means for the World (2012), Edge of Chaos: Why Democracy Is Failing to Deliver Economic Growth – and How to Fix It (2018), na How Boards Work: And How They Can Work Better in a Chaotic World (2021).
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Moyo alizaliwa mwaka 1969 katika Lusaka, Zambia.[1] Sehemu ya utoto wake alikulia nchini Marekani, wakati baba yake alipokuwa akifanya masomo ya juu, kisha akarudi Zambia.[2]
Alisoma kemia katika Chuo Kikuu cha Zambia,[2] na alikamilisha BS yake katika kemia mwaka 1991 katika American University huko Washington, D.C. kupitia ufadhili wa masomo.[1] Alipata MBA katika fedha kutoka chuo hicho mwaka 1993.[3][4]
Alipata Master of Public Administration (MPA) kutoka Chuo Kikuu cha Harvard katika Shule ya Utawala ya John F. Kennedy mwaka 1997.[3][5] Mnamo mwaka 2002 alipata DPhil katika uchumi kutoka Chuo cha St Antony, Chuo Kikuu cha Oxford.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Moyo, Dambisa. "Preface" Archived 2017-03-19 at the Wayback Machine. Dondoo kutoka DEAD AID: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa. Farrar, Straus na Giroux, 2009. Ilichapishwa tena katika The Wall Street Journal, 20 Machi 2009.
- ↑ 2.0 2.1 "Dambisa Moyo". Encyclopædia Britannica. https://www.britannica.com/biography/Dambisa-Moyo.
- ↑ 3.0 3.1 Curley, Robert. "Moyo, Dambisa" Archived 2016-05-19 at the Wayback Machine. Katika: Britannica Book of the Year 2013. Encyclopædia Britannica, Inc., 2013. p. 97.
- ↑ Dambisa F. Moyo BSc, MPA, MBA, Ph.D. Archived 2015-09-24 at the Wayback Machine – Profaili ya Mtendaji katika Bloomberg.
- ↑ Anderson, Lindsay Hodges. "Alumna Argues Aid in Africa is Failing, Needs to be Reassessed" Archived 2011-03-26 at the Wayback Machine. Habari na Matukio ya Harvard Kennedy School. HKS.Harvard.edu. 1 Aprili 2009.
- ↑ Dambisa Moyo Archived 2013-05-20 at the Wayback Machine. Encyclopædia Britannica. Imechukuliwa 19 Mei 2015.