Nenda kwa yaliyomo

Dada Kidawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dada Kidawa - Sister Kidawa
Dada Kidawa - Sister Kidawa Cover
Compilation album ya Mbalimbali
Imetolewa 15 Agosti, 1995[1]
Imerekodiwa Miaka ya 1960-70
Aina Muziki wa dansi
Lebo Original Music


"Dada Kidawa - Sister Kidawa" ni jina la albamu ya nyimbo mchanganyiko ya muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Albamu imekusanya nyimbo za miaka ya 1960-na-1970 na kuziweka pamoja. Albamu ilitolewa tarehe 15 Agosti, 1995. Jina la albamu ni chaguo la wimbo kutoka katika orodha ya nyimbo walizochagua, wimbo umeimbwa na Western Jazz Band. Baadhi ya nyimbo za humu ni pamoja na Naumiya ya Cuban Marimba Band, Muungano Tanzania ya Kilwa Jazz Band, Sisi Vijana Wema ya National Jazz Band, Mpenzi Sema ya Dar es Salaam Jazz Band na Mpenzi Zaina ya Njohole Jazz Band. Kulingana na mhakiki wa masuala ya muziki wa Marekani, Robert Christgau, anasema nyimbo nyingi za miaka ya 1960 za Tanzania zilikuwa zinachukua muundo wa midundo na mitindo ya Kikongo na kuifanya ya Kitanzania.

Ametolea mfano wimbo wa Njohole Jazz Band, "Mpenzi Zaina" na wa Dares Salaam Jazz Band, "Mpenzi Sema".[2] Tabia hii ya kuchukua midundo ya Kikongo na Kuitanzania ilikuwa kawaida sana katika miaka ya 1950 na 1960 mwanzoni. Hadi hapo serikali ilipopiga marufuku kukopi nyimbo za Kikongo, hasa baada ya uhuru ilikuwa lazima watunge nyimbo za kusifu juhudi za serikali na chama tawala wakati huo. Bendi hasa zilizokuwa zinaiga moja kwa moja midundo ya Kikongo Tanzania zilikuwa tatu, DAR Jazz, Western Jazz na Kilwa Jazz. Hizo hasa zilichukua midundo ya Kikongo na kuipiga kwa Kitanzania.

Katika miaka ya 1960 mwanzoni, sehemu kubwa ya wasanii walitunga nyimbo za kuisifu TANU na wanaharakati wa uhuru wa Tanganyika. Baada ya uhuru nyimbo nyingi za siasa zilitungwa. Kuhamasisha kulima, elimu, kuondoa mabalaa ya njaa, nyimbo za kuhamasisha ufanisi kazini, nyimbo za kuhamasisha sera za ujamaa na kujitegemea na kadhalika.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hii.

  1. Salaam Kwa Jumla - Cuban Marimba Band
  2. Tunda Bichi - Kiko Kids Jazz
  3. Naumiya - Cuban Marimba Band
  4. Tanganyika Na Uhuru - Kiko Kids Jazz
  5. Naliya Naliya - Cuban Marimba Band
  6. Kiko Mwanisakama - Kiko Kids Jazz
  7. Sipati Majibu - Cuban Marimba Band
  8. Muungano Tanzania - Kilwa Jazz Band
  9. Nitafurahi Ukitumwa Tena - Western Jazz Band
  10. Mwangele - Nuta Jazz Band
  11. Sisi Vijana Wema - National Jazz Band
  12. Njoo Mpenzi Njoo - Atomic Jazz Band
  13. Mipachangui - Nuta Jazz Band
  14. Mpenzi Sema - Dar es Salaam Jazz Band
  15. Mpenzi Sofia - Nuta Jazz Band
  16. Dada Kidawa - Western Jazz Band
  17. Agwe Tuchole - Nuta Jazz Band
  18. Bwana Mwizi - Nuta Jazz Band
  19. Mpenzi Zaina - Njohole Jazz Band

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Dada Kidawa katika wavuti ya Amazon. Audio CD (August 15, 1995).
  2. Dada Kidawa/Sister Kidawa Original Music, 1995 more '60s dance hits from Tanzania, which improve as they Congo-Cubanize (Njohole Jazz Band, "Mpenzi Zaina"; Dares Salaam Jazz Band, "Mpenzi Sema").