DJ Allyb
Ally Suleiman Simba (anajulikana zaidi kwa jina la DJ Allyb[1] au Profesa[2]; alizaliwa 16 Machi 1986) ni DJ maarufu kutoka nchini Tanzania.
Amekuwa akitumbuiza kumbi na vituo mbalimbali vya redio kwa zaidi ya miaka kumi. Anatambulika zaidi kwa mtindo wake wa upigaji kelele katika akaunti yake ya Instagram kila ifikapo Ijumaa. Siku ambayo huhesabiwa kama starehe za mwishoni mwa wiki huanza. Ally amewahi kufanya kazi na kilabu cha Maisha Basement kwa miaka mitano. Zaidi akisimamia sherehe mbalimbali na kutoa burudani anuwai katika muziki tofauti. Ukiachana na Maisha, Allyb pia amewahi kufanya kazi na vilabu vingine kama vile Laliga (Moshi), TRIPPLE A (Arusha), Rock Bottoms (Mwanza), Elements, High Spirit, Havoc & Buckets ya Dar es Salaam. Mbali na u-DJ Allyb pia ni mtayarishai wa kandamseto mbalimbali, akisanifu shughuli na sherehe mbalimbali.
Kupenda kwake muziki kukapelekea kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa kimataifa. Wasanii hao ni pamoja na DJ MAPHORISA kutoka Afrika Kusini. Pia amewahi kufanya kazi jukwaa moja na Sauti Soul kutoka Kenya, Patoranking na Maleek Berry kutoka Nigeria. Ukiachana na utumbuizaji kwenye sherehe na kumbi mbalimbali, Allyb amewahi pia kufanya kazi na vituo anuwai vya redio ikiwa ni pamoja na Tripple A FM, KISS FM, Passion FM, Times FM, TBC FM na E FM. Pia amewahi kushiriki kwenye kipindi cha runinga kilichokuwa kinarushwa mbashara kupitia matamasha mbalimbali. Moja wapo ilikuwa Extreme Live wakirusha matangazo ya moja kwa moja katika Tamasha la Nyama Choma, Life of the Beach, Mziki Mnene, Wasafi Festival, Three 2 Nine, Budx Party na Castle Lite Unlock kwa Tanzania na Afrika Kusini.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Haikuwa Rahisi: Simulizi ya DJ Ally B - Umaskini hadi kuwa DJ anayelipwa zaidi Tanzania (Part 1), iliwekwa mnamo 2023-03-16
- ↑ Edwin TZA. "Utajiri wa Dj Ally B anaye-trend kwa mizuka ndani ya gari, kasimulia maisha yake, "Nimeishia la saba"". Millard Ayo (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-03-16.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu DJ Allyb kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |