Nenda kwa yaliyomo

Cree Cicchino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Cree Cicchino (alizaliwa 9 Mei 2002) ni mwigizaji wa Marekani.

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Cree Cicchino alikulia huko Glendale, Queens, New York. Yeye ni nusu Ekadoado, nusu Mwitalia. Cree Cicchino ana dada pacha aitwae Joyce Cicchino. Cree Cicchino aliingia kwenye darasa la kucheza wakati akiwa anaumri wa miaka 4, lakini mama yake alimpeleka kwenye darasa la uigizaji wakati akiwa anamiaka 12 baada ya kuamua kuwa muigizaji.

Cree Cicchino alianza kazi yake kama mwigizaji akiwa mdogo akicheza mmoja wa wahusika wakuu katika safu ya Game Shakers kwenye Nickelodeon Archived 17 Julai 2013 at the Wayback Machine., ambayo ilirushwa kutoka 2015 hadi 2019.

Mnamo mwaka 2015 Cree Cicchino akiwa ana miaka 13 alichukuliwa katika jukumu la kuigiza kama Babe katika safu ya Game Shakers ambayo ilichezwa kwa misimu mitatu.

Mnamo Agosti 2018 alipewa jukumu la kuigiza kama Marisol Fuentes kwenye safu ya Mr. Iglesias kwenye Netflix Archived 14 Julai 2013 at the Wayback Machine. ambayo iliachiliwa 2019. Pia Cree Cicchino alipewa jukumu la kuigiza kama Mim kwenye filamu Sleepover ambayo ilitolewa mnamo 2020.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cree Cicchino kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.