Chuo cha Taaluma cha Kisongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo cha Taaluma cha Kisongo ni taasisi ya ushirikiano. Sasa inaendesha shule yake ya kwanza ya sekondari iitwayo Shule ya Sekondari ya KAC iliyo katika Mkoa wa Arusha, Tanzania.

Shule hiyo iko katika Mkoa wa Arusha kaskazini mwa Tanzania, huko Kisongo, kijiji asili cha Wamasai, karibu kilomita 1.2 (maili 0.75) kando ya barabara ya Lekamba, na takriban kilomita 14 (maili 8.7) kutoka mji wa Arusha.

Mwenyekiti wa chuo cha bodi ya ushauri ni Eng. Calvin Marealle, ambaye amefundisha kwa muda mrefu katika Chuo cha Ufundi cha Arusha (Tanzania) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Kigali (Rwanda).[1]

Idara[hariri | hariri chanzo]

Shule ina idara zifuatazo:

1.Idara ya elimu ya sekondari.

2.Teknolojia na mafunzo ya kitaaluma.

3.Kuendelea na elimu.

4.Ujuzi wa lugha na mawasiliano.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. kisongocollege.com
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo cha Taaluma cha Kisongo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.