Chuo Kikuu cha Pwani
Chuo Kikuu cha Pwani ni chuo kikuu ambacho kiko katika eneo ya ekari mia sita karibu na mji wa Kilifi, nchi ya Kenya[1].
Falsafa ya chuo kikuu hiki ni kuwa shule ya “ubunifu, mabadiliko, na usikivu.[2] Kuna shule saba tofauti Chuo Kikuu cha Pwani ambazo wanafunzi wanaweza kusoma masomo mengi tofauti.
Historia ya Chuo Kikuu cha Pwani
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya Chuo Kikuu cha Pwani kuanzishwa, kiliitwa Taasisi ya Kilimo ya Kilifi. Tarehe ishirini na tatu, mwezi wa nane, mwaka wa 2007, Taasisi ya Kilimo ya Kilifi ilibadilishwa na kuwa chuo ambacho kilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Chuo kilifunguliwa na rais wa Kenya, Mwai Kibaki, tarehe mbili, mwezi wa kumi na moja, mwaka wa elfu mbili na saba. Halafu, tarehe thelathini na moja, mwezi wa kwanza, mwaka wa elfu kumi na tatu, chuo kilibadilishwa na kuwa Chuo Kikuu cha Pwani baada ya kupata mkataba.[1]
Masomo na Shule
[hariri | hariri chanzo]Katika Chuo Kikuu cha Pwani, kuna programu za shahada mia moja na kumi jumla. Kuna shahada za kwanza hamsini na tisa[3], shahada za pili ishirini na tisa[4], na shahada za tatu ishirini na mbili[5] ambazo wanafunzi wanaweza kuamua kusoma. Pamoja na programu za shahada hizo, Chuo Kikuu hiki kina programu za cheti nne[6] na programu za stashahada ishirini pia.[7]
Programu za shahada hizo ziko shule saba tofauti Chuo Kikuu cha Pwani. Shule hizo ni:
- Shule ya Sayansi Tumizi na Sayansi Msingi (Mshauri: Mwalimu Bernard Mulwa Fulanda)
- Shule ya Biashara na Uchumi (Mshauri: Mwalimu Abdullah Ibrahim Ali)
- Shule ya Ubinadamu na Sayansi Jamii (Mshauri: Mwalimu Halimu S. Shauri)
- Shule ya Afya na Sayansi ya Binadamu (Mshauri: Mwalimu Makorani Y’Dhida-a-Mjidho)
- Shule ya Elimu (Mshauri: Mwalimu Sammy K. Rutto)
- Shule ya Dunia na Sayansi ya Mazingira (Mshauri: Mwalimu Annie Hilda Ong’ayo)
- Shule ya Sayansi ya Kilimo na Viwanda vya Huduma za Kilimo (Mshauri: Mwalimu Hemedi Mkuzi Saha)[8]
Watu Muhimu
[hariri | hariri chanzo]Kwa utawala wa Chuo Kikuu cha Pwani, Makamu Mkuu anaitwa Mwalimu James H. P. Kahindi. Yeye anafundisha masomo ya mikrobiolojia pale pia, na kabla ya hii, alifundisha masomo ya sayansi asili katika Chuo Kikuu cha Mataifa cha Marekani – Afrika.[9] Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Pwani wingine ni Mwalimu Paul Guyo, Mwalimu Helem Mondoh, na Mwalimu Mlewa C. Mwatete.[10] Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chuo Kikuu cha Pwani anaitwa Mwalimu Mohamed Salim Badamana.[11]
Matukio ya Habari Kuhusu Chuo Kikuu
[hariri | hariri chanzo]Tarehe thelathini, mwezi wa tatu, mwaka wa 2023, basi la Chuo Kikuu cha Pwani ambalo lilikuwa limebebeka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pwani lilipata ajali kwa kugongana na matatu barabarani. Wanafunzi walikuwa wakisafiri kwenda Eldoret ili kutazama mchezo, lakini basi lilipoendeshwa katika barabara ya Nairobi-Nakuru, breki za basi zilishindwa kufanya kazi.[12] Watu kumi na nane walikufa – watu tisa miongoni mwa watu hawa walikuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pwani, na watu wengine watatu walikuwa wafanyakazi chuoni.[13]
Chuo Kikuu cha Pwani kilifunga kutoka tarehe moja mwezi wa nne mpaka tarehe kumi na saba mwezi wa nne ili kuwapa wanafunzi wakati kuhuzunisha wanafunzi waliofariki. Tarehe za mitihani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pwani zilihamwa kuanza tarehe mbili mwezi wa tano na kumaliza tarehe kumi na mbili mwezi wa tano.[13]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Pwani University. 2021. Pwani University students guidebook. http://environment.pu.ac.ke/forms/Students%20Guide%20Book%202021.pdf
- ↑ "Statements". Pwani University (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Bachelors Programmes". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Masters Programmes". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "PhD Programmes". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Certificate Programmes". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Diploma Programmes". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Schools at PU". Pwani University (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ Kahindi, J. H. P. (2016, January). Curriculum Vitae. Pwani University. https://www.pu.ac.ke/profiles/Prof.%20James%20H.%20P.%20Kahindi%20CV%20February%202017.pdf
- ↑ "Administration". Pwani University (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "Governance". Pwani University (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ "At Least 14 Killed After Pwani University Bus Collides with a Matatu in Naivasha". Mwakilishi.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ 13.0 13.1 "Pwani University closed after accident that killed nine students, three staff". Nation (kwa Kiingereza). 2023-04-01. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.