Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Chuka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo kikuu cha Chuka ni chuo kikuu cha umma katika Kaunti ya Tharaka-Nithi, Kenya. Chuo kikuu kiko umbali wa takribani km 186 kutoka Nairobi kando ya barabara ya Nairobi-Meru, katika mazingira ya vijijini kwenye mteremko wa mashariki wa Mlima Kenya kwenye kimo cha takribani mita 2,000 juu ya usawa wa bahari. Chuka University iko ndani ya Jimbo la Chuka/Igamba-ng'ombe, Kaunti ya Tharaka-Nithi.