Lloyd Banks
Lloyd Banks | |
---|---|
| |
Jina Kamili | {{{jina kamili}}} |
Jina la kisanii | Lloyd Banks |
Nchi | Marekani |
Alizaliwa | 30 Aprili 1982, |
Aina ya muziki | Rap na Hip hop |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Miaka ya kazi | 1999 - hadi leo |
Ameshirikiana na | G-Unit, Eminem |
Ala | Sauti |
Kampuni | G-Unit, Interscope |
Christopher Charles Lloyd (Amezaliwa tar. 30 Aprili 1982), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lloyd Banks, ni rapa wa kimarekani na mmoja wa kundi la G-Unit.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Lloyd Banks alizaliwa na mzee Christopher Lloyd mjini Baltimore, Maryland na akakulia mjini South Jamaica, Queens. Mama yake ni Mpuerto Rico na baba yake ni Mmarekani mweusi.
Wakati wazazi wa Banks wangali vijana hawakuwahi kuoana hadi alivyokuja kuzaliwa Banks. Baba yake aliambulia zaidi utoto wa Banks akiwa jela, na kumuacha Banks akilelewa na mama yake huku akiwa anapata msaada kutoka kwa ndugu wa baba wa Banks. Mamam yake Lloyd Banks alikuwa na kawaida ya kumuacha Lloyd akiwa anaangaliwa na kaka yake Lloyd pindi tu mama aendapo mizungukoni
Akiwa mdogo Banks alianza kuandika vitu vinanvyofanana na maishairi na kuanza kuvifanyia mazoezi. Kwa bahati nzuri Lloyd akapata moyo zaidi na kuanza kurap katika baadhi ya mitaa iliyopo mjini New York.
Kwakweli iliwagusa baadhi ya watu na kuanza kumshangaa Lloyd anavyo fanya mambo ya ajabu mtaanii hapo. Akawa anahifadhi baadhi ya mashari kisha anaenda kushiriki katika mashindano ya mtaani, huku akiwa anabuni nanma ya kuwavuta watu, pia na majigambo yasiyozulika na kuanza kujivumisha kuwa yeye ni mmbora zaidi.
Kuja kuwa maarufu
[hariri | hariri chanzo]Tony Yayo, ni mkubwa kiumri na anauzoefu katika muziki wa rap, alijiunga na 50 Cent katika safari ya kumtafutia soko Nas, Cash Money na Ruff Ryders. Banks yeye alibaki nyumbani akimsubiri 50 Cent na Yayo kurudi huko safarini. Banks yeye alianza kuimba mtaani huku akizunguka katika nyumba za majirani huku akizidi kujitamba mtaani.
Baadae alichukuliwa na mtaarishaji mmoja wa muziki wa jirani kwao na kuanza kutengeneza tepu za nyimbo mchanganyiko za kienyeji. Lloyd Banks ameanza kujulikana na kupewa heshima baada ya kutoa sini ya tepu mchanganyiko.
Albamu alizotoa
[hariri | hariri chanzo]Makala kuu ya albamu za Lloyd Banks
- 2004: The Hunger for More
- 2006: Rotten Apple
- 2008: Gang Green
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- http://www.sixshot.com/3684/ Ilihifadhiwa 3 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.sing365.com/music/lyric.nsf/Lloyd-Banks-Biography/BFE96E13A180848B48256EC5000CF234 Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- http://www.g-unitsoldier.com/main.html
- http://www.askmen.com/men/entertainment_150/165c_lloyd_banks.html Ilihifadhiwa 27 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Lloyd Banks katika All Music Guide
- Lloyd Banks at the Internet Movie Database
- Lloyd Banks katika MySpace
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lloyd Banks kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |