Nenda kwa yaliyomo

Chris Okotie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchungaji Chris Okotie

Chris Okotie (aliyezaliwa 16 Juni 1958) amekuwa mchungaji wa kanisa la The Household of God, Lagos, Nigeria tangu Februari 1987. Amegombea kiti cha Rais wa nchi hiyo mara mbili.

Elimu na wasifu

[hariri | hariri chanzo]

Okotie alizaliwa na Francis Idje na Cecilia Okotie, katika eneo la Ethiope-West, Delta State (iliyokuwa ikiitwa Bendel State). Alihudhuria shule za upili ya Edo College, Benin City. Mwaka 1984, alifuzu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nigeria katika Nsukka. Okotie aliachana na kazi ya sheria baada ya chuo kikuu akaanzia kazi ya muziki iliyofana sana. Pamoja na Dizzy K Falola, Jide Obi, na Felix Uhuru aliipa moto kazi ya muziki iliyokuwa imeanza kujitokeza[1]

Wakati kazi yake ya muziki ilikuwa imefana kabisa, alianzia huduma yake ya dini. Okotie alihudhuria shule ya 'Grace Fellowship Bible' na muda mfupi baadaye kuanzisha Kanisa la 'Household of God'.

Okotie ndiye mwanzilishi wa tuzo ya Karis, inayofanyika kila mwaka na iliyoanzishwa mwaka 1990 na kanisa lake. Tuzo hili huwatambua na kuwatuza kifedha, mbele ya wajumbe wa serikali, wananchi wa Nigeria ambao wametumikia taifa bila kujipenda.

Kutalakiana kwake na mkewe Tina na baadaye kumwoa Stephanie Henshaw kumeleta utata mwingi baina ya Wakristo stadi wa Nigeria wanaoamini kuwa talaka si ya Kibiblia.

Okotie aligombea kiti cha Urais mara ya kwanza akitumia tikiti ya chama cha Justice; lakini alishindwa na Olusegun Obasanjo katika uchaguzi mkuu wa Mei 2003. Alijaribu tena mwaka 2007 kama mwanachama wa 'Fresh Democratic' lakini alishindwa na Umaru Yar'Adua katika uchaguzi mkuu wa Mei 2007.

Machapisho

[hariri | hariri chanzo]
  • The Last Outcast (2001)
  1. Adeniji, Olayiwola. "For Dizzy K, a Centre of Joy", Africa News Service, 2002-04-26. Retrieved on 2009-05-23. 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.