Askari farasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cavalry)
Askari farasi Waingereza kwenye mapigano ya Waterloo

Askari farasi (Kiing. cavalry) walikuwa sehemu muhimu ya jeshi katika historia ya vita hadi karne ya 20.

Tangu kupatikana kwa magari ya kivita, matumizi ya farasi, ngamia au punda kwa shughuli za kijeshi yamepungua sana.

Majeshi kadhaa huendelea kutumia jina la "cavalry" kwa vikosi vya vifaru au askari wa miguu wenye magari ya kasi lakini vikosi hivi havitumii farasi tena. Nchi chache huendelea kutunza vikosi vichache vya askari farasi kwa sababu za kihistoria, maonyesho na gwaride.

Watu wamepigana vita juu ya farasi tangu walibuni kupanda farasi. Askari farasi husafiri haraka kuliko askari wa miguu, wanaweza kubeba silaha nzito kuliko askari wa miguu na pia kuvaa mavazi ya kinga nzito zaidi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]