Carmen Batanero
Carmen Batanero ni mwalimu wa takwimu wa Uhispania, na mhadhiri mwandamizi katika Idara ya Hisabati ya Chuo Kikuu cha Granada, Uhispania.[1] Anajulikana kama mtetezi wa elimu ya takwimu.[2] Batanero ni mwanachama wa kudumu wa Chama cha Kimataifa cha Elimu ya Kitakwimu, na aliwahi kuwa rais wa chama kuanzia 2001 hadi 2003.[3] Ameandika kwa ushirikiano makala nyingi za kitaaluma katika nyanja za elimu ya hisabati na takwimu katika miongo miwili iliyopita, na amepewa sifa katika vitabu viwili vya kiada vya takwimu.[4] Michango yake inamweka kama mmoja wa watafiti mashuhuri katika taasisi yake.[5] Dk. Batanero alipata shahada yake ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Granada mwaka wa 1983, kwa tafiti [thesis] ya nadharia Modelos de choque ya exposición intermitente a riesgo de fallo.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martorell-Marugán, Jordi; Tabik, Siham; Benhammou, Yassir; del Val, Coral; Zwir, Igor; Herrera, Francisco; Carmona-Sáez, Pedro (2019-11-01), "Deep Learning in Omics Data Analysis and Precision Medicine", Computational Biology, Codon Publications, ku. 37–53, ISBN 978-0-9944381-9-5, iliwekwa mnamo 2024-04-16
- ↑ Hirst, Joel D.; Sabatini, Christopher (2014-02-01), "¿Qué es la Alternativa Bolivariana para las Américas y cuál es su propósito?", ¿La hegemonía norteamericana en declive?, Editorial Universidad Icesi, ku. 28–40, ISBN 978-958-8357-78-2, iliwekwa mnamo 2024-04-16
- ↑ Technical Committee Guidelines, SAE International, iliwekwa mnamo 2024-04-16
- ↑ Foley, Michael; Kochalko, David (2012-08-15). "Open Researcher and Contributor Identification (ORCID)". Anything Goes. Against the Grain Press. doi:10.5703/1288284314850.
- ↑ GONZÁLEZ, ENRIQUE LUENGO (2015-11-19), "De la insatisfacción metodológica al encuentro con la transdisciplina", Diálogos sobre transdisciplina: Los investigadores y su objeto de estudio, ITESO, ku. 369–394, ISBN 978-607-9473-11-2, iliwekwa mnamo 2024-04-16
- ↑ Dialnet, Universidad de La Rioja (2002-06-30). "Dialnet (Servicio de Difusión de Alertas en la Red)". Contextos Educativos. Revista de Educación. 0 (5): 276. doi:10.18172/con.519. ISSN 1695-5714.