Cape Canaveral
Mandhari
28°28′N 80°32′E / 28.46°N 80.53°E
Cape Canaveral ni rasi ndogo kwenye pwani la Jimbo la Florida katika kusini mwa Marekani. Ni mashuhuri kama eneo ambako makombora na vyombo vya angani vya Marekani vilirushwa.
Katika eneo la Cape Canaveral kuna vituo viwili vinavyohusika na usafiri wa anga:
- Kennedy Space Center (KSC) ya NASA na kutoka hapa vilirushwa vyombo vya angani vya Kimarekani vilivyobeba abiria, kama vile Saturn V na Space Shuttle.
- Kituo cha Cape Canaveral cha jeshi la anga la US Air Force ambako makombora ya kubeba satelaiti na vipimaanga vimerushwa.
Kati ya 1963 hadi 1973 rasi ilibadilishwa jina ikaitwa "Cape Kennedy" lakini baadaye jina la awali likarudishwa.
Rasi hii iliteuliwa kwa ajili ya viwanja vya usafiri wa angani kwa sababu iko katika kusini ya Marekani hivyo karibu zadi na ikweta. Makombora yanahitaji nguvu na fueli kidogo kufika obiti kama yanarushwa karibu na ikweta ya Dunia.