Caoimhín Kelleher

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kelleher akiwa na Liverpool mnamo 2021

Caoimhín Odhrán Kelleher alizaliwa 23 Novemba 1998 ni mchezaji wa kandanda kutoka nchi ya Eire (Ireland) ambaye anacheza kama golikipa wa Liverpool na timu ya taifa ya Jamhuri ya Eire.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Kelleher alizaliwa Cork, katika kaunti ya Cork,[1] ambapo alihudhuria chuo cha Presentation Brothers.[2]

Maisha ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Kelleher alijiunga na akademi ya Liverpool kutoka Ringmahon Rangers majira ya joto 2015. Alishiriki mara kadhaa na kuwepo kwenye kikosi cha Liverpool wakati wa programu yao ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya ziara ya Liverpool majira ya kiangazi..[3]

Mnamo Agosti 2018, alisaini mkataba mpya na Liverpool.[4] Alikuwa miongoni mwa wachezaji wasiotumika wa benchi la Liverpool Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA 2019 walipocheza dhidi ya Tottenham Hotspur.[5] Katika kushinda Ligi ya Mabingwa, alikua mwanasoka wa 12 wa Eire kufanya hivyo na wa kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]