Nenda kwa yaliyomo

Candace Owens

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Candace Owens

Candace Owens, (alizaliwa Stamford, Connecticut, 29 Aprili 1989) ni mchambuzi wa kisiasa wa Marekani ambaye ana uhusiano wa karibu na Donald Trump na tangu mwaka 2017 amekuwa akijihusisha na harakati za kihafidhina.[1] Owens anajulikana kama mpinzani wa hadhara wa harakati za Black Lives Matter na pia ni mpinga utoaji mimba.[2]

Owens ameibua utata kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono Vladimir Putin wakati wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Aidha, amekuwa maarufu kwa kutoa au kuunga mkono kauli zenye ukosoaji dhidi ya Wayahudi, kueneza nadharia za ukanushaji wa historia, kauli za chuki dhidi ya watu wa jinsia moja, na nadharia za njama.[3]

  1. "Prononciation de l'anglais", Wikipédia (kwa Kifaransa), 2024-07-25, iliwekwa mnamo 2024-09-20
  2. Nagle, Angela (2017-11-14), "The Lost Boys", The Atlantic (kwa Kiingereza), ISSN 2151-9463, iliwekwa mnamo 2024-09-20
  3. Mallory Shelbourne (2018-05-09). "Trump praises conservative activist Candace Owens as a 'very smart thinker'". The Hill (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-20.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Candace Owens kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.