Camembert (jibini)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Camembert.

Camembert ni jibini laini kutoka Ufaransa. Asili yake iko katika jimbo la kutoka Normandi) kwenye kijiji cha Camembert.

Jibini hii inatengenezwa kwa maziwa ya ng'ombe isiyochemshwa na kuvu ya Camembert (Penicillium camemberti). Inaiva angalau wiki 3 ikifunikwa na ganda la fuvu kabla ya kufungwa katika karatasi na kuuzwa. Hutengenezwa kwa umbo la donge mviringo zenye takriban gramu 250.

Camembert changa ni gumu kiasi lakini kadri inavyozidi kuiva inalainika na kupata ladha ya pekee. Ikikaa muda mrefu ladhaa inaweza kuwa kali na watu wengine wanaipenda vile lakini wengine huona inanuka.