Nenda kwa yaliyomo

Béjaïa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Béjaïa (wakati wa ukoloni wa Ufaransa ulijulikana kama Bougie au Bugia[1]) ni mji wa bandari kwenye ghuba ya Béjaïa nchini Algeria; ni mji mkuu wa Wilaya ya Bejaia, Kabylia. Béjaïa ni mji mkubwa zaidi unaotumia lugha ya Tamazight.

Mji huo unatazamana na mlima Yemma Gouraya ambapo mwonekano wake unafananishwa na umbo la mwanamke aliyelala. Maeneo mengine ya karibu ni pamoja na pwani ya "Aiguades" na "Pic des Singes" (Monkey Peak); hapo wako nyani aina ya Barbary Macaque walio hatarini kukoma. Sehemu hizo zote ziko katika Hifadhi ya Kitaifa ya Gouraya. Mto Soummam unapita katikati ya mji.

  1. "Bougie (n)". Oxford English Dictionary. Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 29 Novemba 2012. Etymology: < French bougie wax candle, < Bougie (Arabic Bijiyah), a town in Algeria which carried on a trade in wax{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Available online to subscribers

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Béjaïa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.