Nenda kwa yaliyomo

Benjamin Fernandes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Benjamin Fernandes (amezaliwa 25 Novemba 1992) ni mjasiriamali wa Tanzania aliyewahi kuwa mtangazaji wa runinga.

Alifanya kazi katika kampuni ya The Bill and Melinda Gates Foundation iliyopo nchini Marekani. Alikuwa Mtanzania wa kwanza[1] kusoma Stanford Graduate School of Business kama Africa MBA Fellow [2] na mdogo kabisa kiumri kukubaliwa katika chuo cha Stanford Graduate School of Business.

Mnamo mwaka 2017 alifanikiwa kuwa Mtanzania wa kwanza kujiunga na masomo katika chuo cha Stanford Graduate School of Business na pia Harvard John F. Kennedy School of Government.[3]

Fernandes ni mwanzilishi wa NALA, jukwaa la kidigitali nchini Tanzania linalowezesha watu kufanya miamala ya kifedha bila kuuunganishwa kwenye mtandao maarufu kama intaneti[4]. NALA inakuwa kwa kasi ambapo imeendelea kuwa katika nchi kadhaa Afrika na nje ya Africa[5].

  1. Qorro, Edward (2015-08-23). "FEATURE : Young Tanzanian's journey to the prestigious Stanford - News". The Citizen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-18. Iliwekwa mnamo 2016-09-01.
  2. "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-18. Iliwekwa mnamo 2016-09-01.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link)
  3. "Tanzanian making history in America at Harvard University". www.ippmedia.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo 25 Machi 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. https://www.ippmedia.com/en/news/meet-tanzania-genius-pioneering-offline-digital-app-payments
  5. https://www.nala.money/
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benjamin Fernandes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.