Nenda kwa yaliyomo

Bendera ya Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Uingereza
Bendera ya Uingereza kama sehemu ya Bendera ya Ufalme wa Muungano wa Britania

Bendera ya Uingereza ni msalaba mwekundu kwenye uga nyeupe. Msalaba ni ya aina ya Mt. George yaani mikono yake hukutana katikati.

Msalaba wa Mt. George humkumbusha mtakatifu huyu wa historia ya Ukristo anayesemekana amemwua joka. Ndiye mtakatifu wa kitaifa wa ulinzi wa Uingereza.

Hasa wanajeshi walioshiriki katika vita ya msalaba wakati wa karne 11-13 BK walipendelea msalaba wake kama bendera yao. Tangu siku zile alama hii ilijulikana sana ikawa bendera ya Uingereza tangu karne ya 13.

Tangu mwaka 1606 bendera za Uingereza na Uskoti ziliunganishwa kuwa bendera jipya la muungano au "Union Jack".