Bendera ya China

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Jamhuri ya Watu wa China

Bendera ya Jamhuri ya Watu wa China ilionyeshwa rasmi mara ya kwanza tar. 1 Oktoba 1949 baada ya ushindi wa Wakomunisti juu ya Kuomintang katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China.

Bendera ni nyekundu ikionesha nyota tano za dhahabu. Nyota kubwa inamaanisha utawala wa chama cha kikomunisti.

Nyota nne ndogo ni za tabaka nne zilizotakiwa kubeba mapinduzi:

  • wafanyakazi
  • wakulima
  • raia wa kawaida
  • mabepari wenye nia ya kujenga taifa