Bendera ya Brazil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Brazil
Bendera ya Dola la Brazil 18 Septemba 1822 - 15 Novemba 1889

Bendera ya Brazil ni ya rangi kijani yenye msambamba sawa njano ndani yake. Ndani ya msambamba sawa kuna duara ya buluu yenye nyota nyeupe ndani yake. Mlia mweupe unakata duara ya buluu mwenye maandishi ya maneno ya wito la taifa "Ordem e Progresso" ("Utaratibu na Maendeleo") kwa herufi za kijani.

Bendera hii inaitwa "Auriverde" yaani "dhahabu-kijani".

Bendera hii imekuwa bendera rasmi tangu 19 Novemba 1889 baada ya mapinduzi yaliyomaliza utawala wa Kaisari ya Brazil na kuanzisha jamhuri. Muundo wake hufuata muundo wa bendera ya kifalme.

Nembo la Kaisari iliondolewa. Badala yake duara ya buluu pamoja na nyota iliingizwa. Duara hii ni picha ya anga la usiku juu ya Rio de Janeiro tarehe 15 Novemba 1889 iliyokuwa siku ya kutangazwa kwa jamhuri.

Mwaka 1992 muundo ulibadilishwa kidogo kwa kupunguza idadi ya nyota. Sasa kila nyota ni ishara ya jimbo moja la kujitawala ndani ya shirikisho la jamhuri hivyo idadi ya nyota ni sawa na idadi ya majimbo la. Lakini nyota zote zinazoonyeshwa ziko mahali pao kulingana na picha ya anga ya tarehe 15.11.1889.