Nenda kwa yaliyomo

Beata Habyarimana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Beata

Beata Uwamaliza Habyarimana (amezaliwa Septemba 1975) ni mchumi na mshauri wa masuala ya kifedha kutoka nchini Rwanda. Uga ambao anautumikia kwa zaidi ya miaka 16 ya uzoefu katika sekta ya fedha na taasisi za ndani ya Afrika na kimataifa. Eneo lake la umahiri linahusisha kubadilisha biashara na mabadiliko ya shirika.

Hivi sasa ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bank of Kigali Group, taasisi kubwa ya kifedha nchini Rwanda yenye kampuni tanzu tano: huduma za Benki, Bima, Usimamizi wa Mali, Suluhisho za Kidijitali kupitia Techouse, na shughuli za Kifilantropia kupitia Asasi yao ya kiraia.[1]

  1. Akayezu Jean de Dieu (2021-07-18). "Umunyakuri wakabije inzozi, iby'igitabo cyamuhinduye: Byinshi ku buzima bwa Minisitiri Habyarimana (Video) - IGIHE.com". igihe.com (kwa Kinyarwanda). Iliwekwa mnamo 2024-12-29.