Baharia Sindbad
Mandhari

Baharia Sindbad (pia: Sinbad; Kar. السندباد البحري as-Sindibād al-baḥri; Kaj.: سندباد Sandbād) ni jina la baharia shujaa wa hadithi kadhaa katika mkusanyo wa fasihi ya Kiarabu unaopatikana katika kitabu cha Alfu Lela U Lela (Usiku Elfu na Moja). Katika hadithi hizo Sindbad ni mtu wa mji wa Basra (Iraki ya leo) wakati wa Ukhalifa wa Waabbasi na hasa khalifa Harun al-Rashid.
Hadithi ya Sindbad zinasimulia habari za safari zake saba kwenye bahari upande wa mashariki wa Afrika na kusini za Asia. Katika safari hizi anakutana na maajabu mengi, madubwana na kupita kwenye hatari nyingi.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Story of Sindbad The Sailor Ilihifadhiwa 20 Desemba 2020 kwenye Wayback Machine.
- 21 Illustrations by the German cartoon pioneer Stefan Mart, from Tales of the Nations (1933) Ilihifadhiwa 16 Februari 2020 kwenye Wayback Machine.