Backgammon
Backgammon ni mchezo wa ubao unaochezwa na watu wawili. Kila mchezaji anatembeza kete zake kwenye ubao. Anatumia dadu 2 kuamulia idadi ya hatua kwa kila kete. Mshindi ni huyu anayemaliza kupeleka kete zote hadi mwisho wa njia na kutoka ubaoni.
Wachezaji wanatofautishwa kwa rangi ya kete ambazo kwa kawaida ni nyeusi na nyeupe.
Ubao wa backgammon na kete
[hariri | hariri chanzo]Ubao huwa na umbo la mchemraba mwenye nusu mbili za chini na juu. Kila upande kuna pembetatu 12, jumla 24 zinazoitwa nukta ("point"). Kati ya nukta ya 6 na 7 kila upande kuna mstari unaotenganisha eneo la nyumbani na la nje.
Kwa mchezaji mmoja chanzo ni nukta ya kwanza chini upande wa kulia, kwa mpinzani wake ni nukta ya kinyume juu. Anayeanza chini anafuata mwendo wa saa, mwenzake kinyume cha saa.
Kete zinapangwa mwanzoni kwenye nukta ya kwanza kila upande 2, wenye nukta ya kumi na mbili 5, kwenye nukta ya kumi na saba 3 na kwenye nukta kumi na tisa 5.
Nukta ya kwanza ya mchezaji ni pia nukta ya mwisho wa mpinzani wake.
Dadu zina pande sita, mchezo unahitaji dadu mbili, ama kwa kila mchezaji au dadu mbili za kushirikiana.
Shabaha ya mchezo
[hariri | hariri chanzo]Shabha ya mchezo ni kufikisha kete zote kwenye nukta ya mwisho wa mzingo halafu kuziondoa kwa njia ya kupiga dadu, kabla ya mpinzani ametimisha kazi hii ka kete zake.
Mchezo
[hariri | hariri chanzo]Katika ufunguzi kila mchezaji anapiga dadu moja mara moja. Mwenye pointi zaidi anaanza. Anapeleka kete moja mbele idadi ya hatua za dadu yake na dadu ya mpinzani pamoja. Kama mchezaji moja amepiga 5 na mpinzani 3, huyu mwenye 5 anaanza. Anapeleke kete ya kwanza hatua 5+3=8.
Baaad ya ufunguzi wachezaji wanapiga dadu mbili kila mmoja kwa zamu.
Mchezaji anaweka kete kulingana na pointi za dadu. Kama amepiga 5+2 anaweza kuweka kete mbili, moja hatua 5 na nyingine hatua 2, au kete moja hatua 5, halafu 2.
Kete zinatembea kuanzia nukta ya kwanza kupitia eneo la nje hadi kuelekea eneo la nyumbani. Keta inaweza kufika nukta kama hii haikushikwa tayari. Nukta imeshikwa kama kete mbili au zaidi ya mpinzani ziko tayari mle. Kama iko kete moja ya mpinzani pekee kete haikushikwa bado, inawezekana kuingia.
Kama haiwezekani kutumia ponti za dadu zote mbili (kwa sababu nafasi zimeshashikwa) pointi za dadu ya juu zinatangulia. Kama pointi zote haiwezekani, mchazaji anapumzika.
Kupiga kete
[hariri | hariri chanzo]Kama kete inafika kwenye pointi penye kete moja ya mpinzani kete hii imepigwa yaani inaondolewa kwenye ubao. Kete iliyopigwa inaweka katikati ya ubao. Mchezaji wake anahitaji kwanza kurudisha kete ubaoni kabla ya kuendelea na kete nyingine.
Kumaliza
[hariri | hariri chanzo]Wakati kete zote 15 zimefika kwenye pointi yoyote za eneo la nyumbani mchezaji anaanza kuzitoa. kwa hii anahitaji kupata dadu zinazolingana na hatua hadi nukta ya mwisho +1, au kubwa zaidi.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.backgammon-fr.com Ilihifadhiwa 8 Februari 2014 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)