Ayigbe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ayigbe ni vitafunio vya nchini Ghana.

Biskuti za Ayigbe.

Katika kutengeneza biskuti hiyo unachanganya pamoja wanga ya muhogo, nazi, sukari, chumvi na maji; baada ya mchanganyiko huo kuweka kwenye oveni ili kuoka kwa joto fulani. Biskuti ikawa na rangi ya hudhurungi nyeupe baada ya kuoka kabisa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Biskuti hiyo ilitengenezwa na Yonunawo Kwami Edze kutoka Agbozome katika Mkoa wa Volta[1]. Yonunawo Kwami Edze alianzisha biskuti kwa jamii ya Agbozome aliporudi kutoka Cote d'Ivoire kama mwokaji mikate mnamo 1907. Aliweza kutumia ujuzi aliojifunza kutengeneza biskuti ya Ayigbe ambayo inafurahiwa na Waghana hadi sasa.

Vitafunio hivi vinaweza kumudu kiuchumi kwa sababu aliwafunza wanawake wengi jinsi ya kuandaa biskuti ili kujikimu kimaisha.[2][3][4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://mobile.ghanaweb.com/GhanaHomePage/features/Ayigbe-biscuit-Yes-we-can-241556
  2. "Ayigbe biscuit: Yes we can!". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). 11 June 2012. Iliwekwa mnamo 2020-06-14.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  3. "AYIGBE BISCUIT A MUST TRY GHANAIAN GLUTEN-FREE STREET SNACK". www.ghanafoodnetwork.net. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-14. Iliwekwa mnamo 2020-06-14.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. "Ayigbe Glutenfree Cassava Coconut Cookie". Savourous (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-06-14. 
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ayigbe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.