Nenda kwa yaliyomo

Attack on Titan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Attack on Titan ni mfululizo wa manga wa Kijapani ulioandikwa na kuchorwa na Hajime Isayama. Hadithi hii imewekwa katika ulimwengu ambapo wanadamu wanalazimika kuishi ndani ya miji iliyozungukwa na kuta tatu kubwa zinazowalinda dhidi ya viumbe wakubwa wanaokula watu, wanaojulikana kama Titans[1].

Hadithi inamfuata Eren Yeager, kijana aliyeapa kuwaangamiza Titans baada ya mji wake kushambuliwa na kifo cha mama yake. Mfululizo huu ulianza kuchapishwa katika jarida la kila mwezi la Bessatsu Shōnen Magazine linalomilikiwa na Kodansha kuanzia Septemba 2009 hadi Aprili 2021. Sura za manga hii zilikusanywa na kuchapishwa katika juzuu 34 zatankōbon.

  1. Valdez, Nick (Mei 10, 2021). "Attack on Titan Creator Discusses the Finale's Most Difficult Decision". Comicbook.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 10, 2021. Iliwekwa mnamo Mei 10, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Attack on Titan kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.