Nenda kwa yaliyomo

Arthur Aaron (mwanasoka)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arthur Frederick Aaron (21 Septemba[1] 1885 - 10 Aprili 1950) alikuwa mchezaji wa kandanda raia wa Uingereza ambaye alicheza katika klabu ya Stockport County. Kialfabeti Arthur Aaron ni mchezaji wa kwanza kwenye orodha.

Aaron alizaliwa  Liverpool, Wazazi wake ni Thomas Aaron na Mary Ann Conroy, pia alikuwa Mkatoliki aliyebatizwa katika kanisa la Our Lady of Immaculate Conception.

Baada ya kustaafu kandanda aliamia kwenye uwakala wa mali zisizohamishi huko Lancashire. Mwaka 1912 alifunga pingu za maisha na Mary Sophia Fleetwood.

Kupitia kura ya maoni ilipofika mwaka 1937, alibadilisha jina lake la ukoo na kuwa Arron.[2] Alifariki akiwa na miaka 64 huko Prescot, Lancashire.

  1. Taarifa za ubazito zinaonesha alizaliwa tarehe 22 mwezi wa 9 mwaka 1939, lakini kwenye msalaba wa kaburi lake unaonesha tarehe 21 mwezi wa 9.
  2. "Page 7321 | Issue 34456, 19 November 1937 | London Gazette | The Gazette". www.thegazette.co.uk. Iliwekwa mnamo 2024-07-27.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Arthur Aaron (mwanasoka) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.