Anti-Virus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Logo ya Vinega au Anti-Virus.

Anti-Virus (vilevile Unti-Virus, Vinega wa Anti-Virus) lilikuwa jina la kutaja mapambano au harakati (movement) ya wasanii wa muziki wa hip hop kudai haki zao za msingi ambazo walikuwa wakizipigania dhidi ya kile walichokuwa wakifanyiwa na baadhi ya vyombo vya habari vyenye nafasi au fursa kubwa kwa wasanii wa muziki wa aina mbalimbali nchini Tanzania. Lengo kuu, ilikuwa kupigania uhai wa muziki wa hip hop ambao ndiyo zao la muziki wa Bongo Flava.

Kulingana na Mkoloni, siku moja taasisi moja kubwa nchini waliitisha kikao na waandishi na baadhi ya washika dau katika tasnia ya muziki, mmoja wa wasimamizi wakuu wa taasisi maarufu nchini alilopoka kuwa anatahakikisha muziki wa hip hop ya Tanzania unakufa. Jambo hili, lilitoka kama mzaha, lakini halisi halisi ndivyo ilivyokuwa kwa kipindi hicho. Tangu kikao kile, Mkoloni na baadhi ya wasanii walikubaliana kuandaa kitu ambacho kita kinzana na mawazo yale. Ili kufanikisha, ilibidi waandae tamasha ambalo litaleta hamasa dhidi ya kauli kama zile za taasisi kubwakubwa. Dhumuni hasa ilikuwa kuwakwamua wasanii wa muziki mbalimbali kutoka mikononi mwa kikundi fulani ambacho kinaonekana kudhibiti mzunguko mzima wa muziki wa Tanzania.

Harakati zilianza kabla ya kumshirikisha Sugu katika dambwe hili. Kama kikosi, walimfuata Sugu na kumueleza juu ya harakati yao. Sugu aliunga mkono harakati, maana tangu zamani yeye alikuwa msema kweli kabla hata ya hiii harakati. Jambo ambalo lilimvutia kuona kwamba kuna watu wanathubutu kukemea udhalimu. Awali Sugu katika wimbo wake wa "Moto Chini" alikemea mno mambo ya media kuhodhi wasanii.[1] Pamoja na harakati hizi kutamba karibia miaka kadhaa tangu kuanzishwa, bado hakuna picha kamili kama kweli wameelewana na hicho chombo kinachodaiwa kuhujumu wasanii au la. Lakini kumekuwa na mazungumzo kati ya Sugu na Ruge na kuafikiana katika kusaidiana na kusapotiana kikazi.[2]

Baadhi ya wanachama[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya wanachama wa Vinega pichani.

Vinega wana orodha kubwa, lakini hii ni baadhi yao tu.

Baadhi ya nyimbo kutoka kandamseto ya Unti-Virus[hariri | hariri chanzo]

 • Antivirus
 • Bado Naua
 • Clouds Get Money
 • Ebwana Inakuaje
 • F.A. na Fala
 • Fleva Zimekwisha
 • "Hello Wafu FM"
 • Huu Mziki
 • Ishu Bado

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Video ya Vinega harakatini na Abby Sykes mnamo tarehe 5 Oktoba, 2011.
 2. Bifu la Vinega laisha makala ya picha na maelezo katika blogu ya Mjumbe.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]