Anne Brodsky

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Anne Ellen Brodsky alizaliwa Juni 11, 1965, nchini Marekani. ni Profesa katika idara ya saikolojia na Gender and Women's Studies katika Chuo Kikuu cha Maryland, Baltimore County (UMBC). Pia, ni Mkurugenzi wa Programu ya Gender and Women's Studies, na Mwenyekiti wa Idara ya Saikolojia. Pia, ameandika kitabu kiitwacho, "With All Our Strength: The Revolutionary Association of the Women of Afghanistan."

Brodsky ni binti wa Allan J. na Clementine Brodsky wa Shaler Township, Pennsylvania. Alihudhuria Shaler Area High School na alipata shahada yake ya kwanza (B.A.) kutoka Chuo Kikuu cha Vassar, Shahada ya Uzamifu (M.A.) kutoka Chuo Kikuu cha Maryland, na Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) kutoka Chuo Kikuu cha Maryland, na aliendelea na masomo ya baada ya uzamivu kutoka Shule ya Afya ya Umma ya Johns Hopkins.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Shaler: Anne Ellen Brodsky", News Record, January 15, 1996, p. 4. Retrieved on August 3, 2018. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anne Brodsky kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.