Aníbal Ibarra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anibal Ibarra: mwanasheria na mwanasiasa wa nchi ya Argentina

Anibal Ibarra (alizaliwa 1 Machi 1958) ni mwanasheria na mwanasiasa wa Argentina kutoka eneo la Lomas de Zamora, wilaya iliyo katika eneo kusini ya Gran Buenos Aires. Alifanya kazi kama mwendesha mashtaka katika mahakama, lakini alijiuzulu kazi hii ili kushiriki katika siasa.Akajiunga na chama kilichokuwa kikianzishwa: the Front for a Country in Solidarity(FrePaSo).

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Ibarra akaanza siasa kwa kuwa mwanachama katika baraza. Katika mwaka wa 2000, alichaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Autonomous Buenos Aires katika duru ya kwanza, akimshinda Domingo Cavallo, aliyekuwa Waziri wa Uchumi wa nchi. Katika mwaka wa 2003, alichaguliwa tena kuwa Meya, akishinda duru ya pili ya kurudia uchaguzi dhidi ya mfanyabiashara Mauricio Macri. Yeye alikuwa ameuungwa mkono na rais mpya aliyechaguliwa, Néstor Kirchner.

Tarehe 30 Desemba 2004, moto katika klabu ya República Cromagnon ulisababisha vifo vya watu 194 na kuzua utata na wimbi la shutuma kwa viongozi wa kisiasa wa mji. Ibarra alishtakiwa wa kupuuza usalama, kutokuwa na uangalifu wa sheria za usalama, kutoendesha shughuli za kuokoa watu vizuri na mashtaka mengine. Tarehe 14 Novemba 2005, tume ya mashtaka iliundwa na tume ya Bunge la Buenos Aires na kumwachisha kazi kwa miezi minne. Alishutumu upinzani kwa kutumia familia za waathiriwa wa moto ya República Cromagnon ili kuharibu wasifu wake wa kisiasa. Alipoachishwa kazi kwa miezi minne hakujiuzulu bali alingoja uchunguzi umalizwe. Wakati huo,Tawi Kuu la Buenos Aires liliongozwa na naibu wa meya Jorge Telerman.

Daniel Filmus ,aliyeshindwa katika uchaguzi wa meya,aliuungwa mkono na Anibal Ibarra

7 Machi 2006,tume ya mashtaka ilitoa hukumu ya kufukuzwa kwa Ibarra kama meya wa Buenos Aires. Kati ya wanachama 15 wa tume hiyo, wanachama 10 walipigia kura kufukuzwa kwa Ibarra,wanne walipinga na mmoja hakupiga kura. Waliomshtaki walitaka apigwe marufuku kwa miaka 10 kutoka kufanya kazi yoyote katika sekta ya huduma kwa raia lakini wanachama wa tume waliamua miaka sita ndio ingetosha. Hapo baadaye wakashindwa kufanya uamuzi kama wampige marufuku au la. [2] [3]

Katika uchaguzi wa mji wa 2 Juni 2007,orodha ya Ibvarra ya sheria za mji ilichukua nafasi ya pili.Yeye na wanachama wengine wa muungano wake - the Popular Progressive Front - wakachaguliwa katika muhula mpya uliyoanza 10 Desemba 2007 huku wakiuunga mkono mgombeaji wa kiti cha meya ,Daniel Filmus.

Dada yake,Ibarra, Vilma Ibarra, ninaibu wa kitaifa na seneta wa zamani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Bloomberg, 7 Machi 2006. Buenos Aires Mayor Ibarra afukuzwa baada ya moto kwa klabu
  2. ^ La Nación, 7 Machi 2006. Destituyeron a Ibarra. Archived 7 Februari 2008 at the Wayback Machine.Lugha ya kihispania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]