Nenda kwa yaliyomo

Amfibia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amphibian)
Amfibia
Chura-sugu wa Garman
Chura-sugu wa Garman
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Kladi: Craniata (Wanyama wenye fuvu)
Nusufaila: Vetebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli ya juu: Tetrapoda (Wanyama wenye miguu minne)
Ngeli: Amphibia
Ngazi za chini

Nusungeli 2, oda ya juu 1, oda 2 na kladi 1:

Amfibia ni kundi la wanyama wenye uti wa mgongo na damu baridi ambao wanaanza maisha kwenye maji na baada ya kupita metamofosi wanaweza kuendelea kwenye nchi kavu katika kipindi cha pili cha maisha yao. Vyura, salamanda na nyoka wanafiki wamo katika ngeli hii.

Jina la kisanyansi "amfibia" linaunganisha maneno mawili ya Kigiriki ἀμφί amphi yaani "pande zote mbili" na βίος bios yaani "maisha" kwa jumla "maisha pande zote mbili" yaani ndani ya maji na kwenye nchi kavu.

Chanzo cha maisha yao ni mayai yaliyotegwa kwenye maji. Amfibia mdogo anatoka kwenye yai katika umbo la ndubwi anayeishi ndani ya maji bila miguu na kupumua kwa yavuyavu ikiwa na mkia. Inaendelea kubadilika na kukuza miguu hadi kutoka kwenye maji ma kufikia umbo la mnyama mzima anayepumua kwa mapafu.

Spishi chache zimeendelea na zinaweza kuzaa bila maji. Wadogo wanafikia umbo la ndubwi na kuendelea na metamofosi ndani ya yai hadi kutoka kwa umbo mzima. Spishi kadhaa zinatunza mayai ndani ya mwili hivi zinazaa wadogo hai.

Amfibia ni wala nyama wanakula viumbe vidogo hasa wadudu.

Kuna takriban spishi 5,700 za amfibia.

Mwainisho

[hariri | hariri chanzo]
  • Ngeli Amphibia
    • Nusungeli Temnospondyli (wameisha sasa)
    • Nusungeli Lissamphibia
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amfibia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.