Nenda kwa yaliyomo

Allan Wanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Allan Wanga
Maelezo binafsi
Jina kamili Allan Wetende Wanga
Tarehe ya kuzaliwa 4 Aprili 1987
Mahala pa kuzaliwa    Kisumu, Kenya
Timu ya taifa
2007-2009 Kenya

* Magoli alioshinda

Allan Wanga akichezea timu ya taifa

Wetende Allan Wanga (alizaliwa Kisumu, 26 Novemba 1985) ni mchezaji wa kandanda wa Kenya, hivi sasa anacheza katika timu ya Atletico Petróleos Luanda nchini Angola. Yeye hucheza katika nafasi ya mshambuliajii katika timu.


Maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake, Frank M. Wetende, alikuwa mchezaji wa AFC Leopards,Kisumu Posta na timu ya taifa kati miaka za 1970 hadi 1980. Mama yake anaitwa Noel Ayieta. Yeye ana ndugu watatu, Richard Malaki, Nancy Kuboka na marehemu Magdalena Amboko.

Watu anaopenda kuiiga mifano yao ni mchezaji wa Parma,Macdonald Mariga, na mshambulizi matata wa Barcelona na Ufaransa,Thierry Henry.

Wasifu wa Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Miaka yake ya ujana

[hariri | hariri chanzo]

Allan Wanga ilianza kucheza soka katika shule ya msingi kama wavulana wote wa umri wake. Akiwa kijana bado alicheza katika ngazi mbalimbali za kiumri katika klabu ya FIFA Kingdom iliyokuwa na makao yake Kisumu lakini sasa imebanduliwa.

Yeye alienda Shule Ya Upili ya St.Paul's, Shikunga katika Wilaya ya Butere na akaendelea kucheza huko, ingawa shule hiyo haikuwa na timu maarufu katika mashindano ya shule za upili.

Wasifu wa Awali

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 2005 alijiunga na Lolwe FC ,iliyo na makao yake Kisumu, ikishirki katika Ligi ya Nationwide(ligi ya zamu ya pili nchini Kenya) Ingawaje, alibaki timu hiyo kwa miezi tatu tu kwa kuwa ligi hiyo ilifungwa ili kuimarishwa na kujengewa miundombinu. Alitengewa mpango wa kujiunga na timu ya Agro Chemical lakini mpango huo haukufaulu kwa kuwa Wanga alitishiwa na wachezaji wa Agro Chemical waliohofia kupoteza nafasi yao katika timu. Yeye,kisha,akaenda nyumbani alikoshawishiwa na mama yake ,Noel, kujiunga na jeshi. Yeye alianguka mtihani wa jeshi lakini akapata nafasi na timu ya Sher Karuturi,mojawapo ya klabu katika Ligi Kuu ya Kandanda nchini Kenya. Alipokuwa akisubiri mkataba na klabu,ndugu yake,Richard,alimtafutia kazi nchini Canada.Allan alijiunga na kaka yake Nairobi ili kuandaa mipango ya kazi hiyo lakini hakufanikiwa kuipata.

Baada ya mwaka mmoja hivi,Lolwe iliwasiliana naye hapo mwaka wa 2006 na akarudi Kisumu.Hapo mwanzo wa mwaka wa 2007, aliajiriwa na klabu ya Ligi Kuu,Tusker FC.Alicheza soka katika timu ya Tusker huku wakishinda ligi mwaka huo.Alikuwa mahiri sana hadi alifunga mabao 13 kwa mechi zake tisa za mwisho ikiongeza hesabu za mabao yake kuwa 21 kwa jumla katika msimu huo.

Wasifu wake akiwa Petro Atletico

[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa 2007, yeye alihamia klabu ya Angola , Petro Atletico, akiwa amekataa nafasi ya kuajiriwa na klabu za Uswidi. Walishinda Ligi Kuu ya Angola (Girabola) katika msimu wake wa kwanza huko,hii ikiwa mara ya kwanza ya Petro Atleticos kushinda tangu mwaka wa 2001.

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Alichezea timu ya taifa,Harambee Stars, kwa mara ya kwanza tarehe 4 Juni 2007 katika mechi na Swaziland. Alifunga bao lake la kwanza akiwa Harambee Stars, alipofunga bao moja dhidi ya Tanzania katika mchuano wa CECAFA 2007.

Katika Kombe la CECAFA 2007, yeye alisaidia timu ya Kenya kuhitimu ngazi ya robo fainali, ambapo wao walishindwa na Uganda katika mikwaju ya penalti.Wanga alifunga mabao matatu katika mechi nne.

Tusker FC

[hariri | hariri chanzo]

Petro Atletico

[hariri | hariri chanzo]

Kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]

Takwimu ya Wasifu | 2005-06 - Lowle FC Ligi ya Nationwide | 2006-07-Tusker FC katika Ligi Kuu ya Kenya | 2008 hadi sasa-Petro Atletico Ligi Kuu ya Angola

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Allan Wanga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.