Ali bin Muhammad
Ali bin Muhammad alikuwa kiongozi wa uasi wa watumwa wa Zanj katika Iraki ya kusini wakati wa karne ya 9 BK.
Habari zake zajulikana kutoka kitabu cha 36 cha Tarikh al-Tabari maandishi ya mwanahistoria Mwajemi Muhammad ibn Jarir al-Tabari aliyeandika wakati wa karne ileile historia yake .
Ujumbe wa Ali bin Muhammad
[hariri | hariri chanzo]Ali alikuwa Mwislamu Mshia wa asili ya Kiajemi lakini alidai alitoka katika ukoo wa Ali ibn Abu Talib na Fatimah bint Muhammad. Akaanzisha uasi wa watumwa wa Zanj akiwahotubia kuwa kutendewa kwao na mabwana hakulingana na amri za dini ya Kiislamu. Ali alisema ya kwamba Allah alimtuma kuwaokoa watumwa na kuwaongoza katika jihadi akajitangaza yeye ni mahdi. Akifuata mafundisho ya Wakhariji alihotubia ya kwamba Mwislamu yeyote wa kweli anafaa kuwa khalifa hata mtumwa mweusi.
Kiongizi wa Wazanj
[hariri | hariri chanzo]Katika Septemba 869 uasi ulianza. Kwa miaka iliyofuata Wazanj walishinda majeshi ya khalifa wa Waabbasi. Ali alijenga mji mkuu wake na kuuita al-Mukhtara ("ulioteuliwa").
Mwisho wake
[hariri | hariri chanzo]Baada ya khalifa kuunganisha nguvu zake za kijeshi dhidi ya dola la Wazanj kuanzia mwaka 879 mwisho ulianza kuonekana.
Katika Agosti 883 jemadari wa khalifa al-Muwaffaq aliteka mji wa al-Mukhtara. Ali bin Muhammad aliuawa kichwa chake ikakatwa na kuonyeshwa katika barabara za Baghdad.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti kuhusu uasi wa Wazanj na Ali Archived 14 Desemba 2007 at the Wayback Machine.