Nenda kwa yaliyomo

Akili mnemba ya jumla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Akili bandia ya jumla)
Kielelezo cha akili bandia ya jumla.

Akili mnemba ya jumla (kwa Kiingereza; Artificial General Intelligence au AGI kwa kifupi) ni tafiti za kinadharia ya akili mnemba inayojaribu kuunda programu ya kompyuta yenye utashi wa kibinadamu na zaidi, yenye uwezo wa kujifundisha yenyewe. Lengo la tafiti hii ni kuunda programu ya kompyuta yenye uwezo wa kufanya kazi ambazo haikufundishwa wala kuundwa kwa ajili ya kazi hizo.

Mifumo ya sasa ya akili bandia hufanya kazi chini ya mipaka iliyowekwa na waundaji wake, mfano, mfumo wa akili bandia wa kutambua au kuunda picha hauwezi kutengeneza wavuti.

Akili bandia ya jumla ni harakati ya kuunda mfumo wa akili bandia unaoweza kujiongoza, unaojitambua na wenye uwezo wa kujifunza ujuzi mpya. Wenye uwezo wa kutatua matatizo magumu katika mazingira na muktadha ambao haikufundishwa wakati wa uumbaji wake. [1]

  1. "What is AGI? - Artificial General Intelligence Explained - AWS". Amazon Web Services, Inc. (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akili mnemba ya jumla kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.