Nenda kwa yaliyomo

Afo-A-Kom

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Afo-A-Kom ni sanamu iliyotengenezwa kwa mbao, ni ishara kubwa ya Wakom wa Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Kameruni. Mnamo mwaka 1966 iliibwa kutoka kiwanja cha kifalme cha Kom. Miaka saba baadaye ilionekana katika jumba la sanaa la Marekani, na baada ya mzozo, lilirudishwa kwa Wakom. [1]

Afo-A-Kom, inamaanisha kitu cha Kom (pia Mbang katika lugha ya Kom). Sanamu hilo lina urefu wa sentimita 159 kwa mtu aliyesimama, limevikwa taji na limeshika fimbo, nyuma yake kuna stuli iliyoungwa kwenye vichwa vitatu vya nyati vilivyochongwa. Msingi wa sanamu hilo ni mbao ya iroko. Uso wake umefunikwa kwa shaba na sehemu kubwa ya mwili imefunikwa na shanga nyekundu na bluu. (Tazama kiunga cha Arthemis hapa chini kwa picha mkondoni. Foyn / Fon (mkuu) anatunza sanamu hiyo, na inaashiria "mamlaka ya kifalme kuendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi mfululizo." [2] Mchongaji wa sanamu hii hajulikani hadi leo lakini inakisiwa kwamba Afo-A-Kom ilichongwa na kiongozi wa jadi wa pili (Foyn) wa watu wa Kom mnamo miaka ya 1920. 

Mnamo mwaka 1966, Afo-A-Kom iliibiwa kutoka kwenye shamba lake takatifu huko Laikom (kiti cha watu wa Kom, ambapo mkuu Foyn anakaa) na mmoja wa mabinti wa kifalme, kisha akauzwa kwa dalali ambaye baadaye alimuuza kwa muuzaji wa sanaa ambaye alilipeleka kwa Marekani. [3] [4] Watu wa Kom wanaamini kuwa sanamu la Afo-A-Kom linamiliki nguvu za maajabu na kwamba muda mfupi baada ya kuwasili Marekani, lilianza kuwasumbua wamiliki wake wapya kwa kuharibu kila kitu kilichokuwa karibu nayo. Wamiliki hao wapya wa kimarekani walichukua sanamu hilo na kuitupa baharini lakini walipo rudi walilikuta palepale lilipokuwa. Afo-A-Kom alipelekwa kwenye jumba la sanaa wa New York ambapo aliuzwa kwa karibu milioni 15 za CFA.

Wakati sanamu hiyo ipo kwenye jumba la sanaa ilitambuliwa na mkusanyaji wa sanaa wa kimarekani Warren M. Robbins ambaye alichangisha fedha pamoja na wamarekani wengine [5] kwa kushirikiana na wasomi na matajiri wa Kom waliokuwa wakiishi Marekani kwa lengo la kununua sanamu hilo kutoka Manhattan na walifanikiwa kulinunua kwa kiasi cha chini ya dola za kimarekani $30,000.[6] wakati akirudisha sanamu hilo nyumbani, Robbins alipokewa na Fon wa Wakom Nsom Ngwe, na Rais wa Kameruni wa wakati huo Ahmadou Ahidjo.

  1. Afo-A-Kom.
  2. Ellis, p. 142.
  3. Blakeslee.
  4. Ellis, p. 141-145.
  5. Ellis, p. 145.
  6. Afo-A-Kom.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Afo-A-Kom kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.