Adrian Siaga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adrian Siaga
Jina la kuzaliwa Adrian Adrian Siaga
Alizaliwa 19 Januari 1975, Dar es Salaam
Tanzania
Jina lingine Adiri
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 2006 - hadi leo

Adrian Adrian Siaga au Adiri (amezaliwa 19 Januari 1975) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anafahamika zaidi kama Mhina kutoka katika filamu ya Zinduna iliyoshirikisha baadhi ya nyota maarufu kama vile Ashura Mushi, Emmanuel Mgaya, Mohammed Muki na Hussein Mkiethi. Vilevile Semwali kutoka katika filamu ya Kimela iliyoshirikisha nyota wengine kadhaa, Anna Peter, Mwasiti Madhohari, Juma Chete, Lilian Nyanza, Zubeiri Ramadhani na Faraji Mohammed. Adiri kutoka katika filamu Seuta II na Seuta II itimisho, Moses kutoka katika filamu ya Julia huku akiwa pamoja na Juma Chete, Mukasa Lawrence, Silvia Tairo, Leah Mussa, Shukuru Kilala, Bakari Abdallah, Abdul Mawazo, Winfrida Wilson, Emma Hassan, Paulina Edward na mwisho kabisa Hussein Mkiethi.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adrian Siaga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.