Adhuri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Athuri ni jina la ujumla la kuwaita wanaume wa kabila la Wagikuyu. Mwanaume mmoja huitwa muthuri. Kundi hili maalum huwa na majukumu kadha, baadhi ya haya zikiwemo, kulinda jamaa yake, kuzalisha hasa kwa lengo la kuendeleza jamii, kujiunga na wanaume wengine katika sherehe zao na kadhalika.

Zamani na hata sasa kundi hili lilijulikana hasa katika kutatua migogoro ya jamii. Jukumu hili lilichukuliwa na serikali pindi wakoloni walipofika nchini. Katika mikutano hii wagomvi walishirikishwa katika kutafuta suluhu. Baadhi ya sherehe walizohitajika kuhudhuria ni sherehe ya kamatimu.