Aïn Defla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moja ya maeneo ya Aïn Defla.

Aïn Defla ni mji mkuu wa jimbo la Aïn Defla, Algeria. [1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Enzi za Dola la Roma mji huo uliitwa Oppidum Novum na mabaki ya Oppidum Novum bado yanaonekana.

Jiji la sasa lilianzishwa katika karne ya 20 na askari aliyeitwa youcef afg wa cheo cha agha, akiwa na wazo la kukusanya watu wa kiasili kutoka vijiji vya mkoa huo.

Eneo hili lisilo tambalale, ambalo lilifikiriwa kuwa sio tulivu kiusalama pia hatari na Wafaransa wakati wa Vita vya Algeria, kwa sababu hio lilitangazwa kuwa eneo lililokatazwa.

Katika miaka ya 1990, mkoa huo huo ulikuwa ngome ya Kikundi cha Waislamu chenye Silaha (GIA). [2] Kulikuwa na mapigano kati ya wanamgambo na wanajeshi wa serikali mnamo Januari 2021 . [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aïn Defla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.