Nenda kwa yaliyomo

116 Clique

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
116 Clique
Aina ya muziki Nyimbo za Kikristo za aina ya Hip Hop
Miaka ya kazi 2005 hadi sasa
Studio Reach Records
Tovuti http://www.reachrecords.com/
Wanachama wa sasa
Lecrae
Trip Lee
J'Son
Sho Baraka
Tedashii
This'l
The Street Disciple
Shai linne
FLAME
Dillon Chase
1-Lyfe
Mmoja wa wasanii wa kundi hili, Lecrae akiimba katika tamasha
Trip Lee

116 Clique ni kundi la muziki la aina ya hip hop ya Kikristo linalotoka Dallas, Texas.Kundi hili huwa na mkataba wa kurekodi muziki zao na studio ya Reach Records. Kundi hili huhusisha wasanii ambao wengi wao hurekodi katika studio za Reach Records. Kundi hili linatoa jina lao la 116 Clique kutoka mstari wa Biblia haswa Warumi 1:16. Mstari huu huzungumza kuhusu kutokuwa na aibu katika Injili kwa sababu ya uwezo wa Mungu huleta ukombozi wa yeyote anayeamini: kwa Myahudi kwanza na pia kwa mataifa mengine yote. Hivyo basi, kundi hili hutambua uwezo wa Injili na wao hujaribu kuitangaza na kuitumia katika maeneo yao yote ya maisha. "Tunaweza kuweka maisha yetu kando na kumtumikia na kumtukuza Mungu katika lolote tufanyalo." Baada ya albamu yao ya kwanza ,The Compilation Album(Albamu ya Mkusanyiko) (2005), DJ Primo alirekodi hizo nyimbo hizo tena akizichanganyachanganya na kutoa albamu ya The Compilation Album: Chopped & Screwed: Special Edition. Albamu hii ya kuchanganywa ilitolewa katika mwaka wa 2006 ikihusisha nyimbo nne za kuongezwa. Kundi hili likaenda ziara ya Unashamed katika mwaka wa 2008. Hapo baadaye katika mwaka wa 2009, Lecrae, Tedashii, Sho Baraka, Trip Lee na Flame wakaenda ziara ya Don't Waste Your Life. Mnamo Oktoba 2009 - Novemba wasanii Lecrae, After Edmund, Sho Baraka, Tedashii, na Mikeschair wakazuru katika ziara ya AlteredMinds. LeCrae, Tedashii, Trip Lee, na Sho Baraka ,hivi sasa, wanazuru wakiwa wasanii binafsi.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • The Compilation Album (2005)
  • The Compilation Album: Chopped & Screwed : Special Edition (2006)
  • 13 Letters (2007)
  • Amped (2007)
  • Albamu mpya ambayo haijapewa jina - 2010.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]