Versailles
Mandhari
Versailles ni mji wa Ufaransa karibu na mji mkuu wa Paris mwenye wakazi 86,000 (2004).
Ni maarufu kutokana na jumba la kifalme lililojengwa hapa na mfalme Louis XIV wa Ufaransa alipopeleka mji mkuu hapa kutoka Paris. Jumba hili lilikuwa baadaye kielelezo kwa majengo ya wafalme kote Ulaya.
Versailles ilikuwa pia mahali pa mikutano muhimu ya kihistoria:
- Tar. 18 Januari 1871 watawala wa Ujerumani walikutana hapa wakati wa Vita ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani wa 1870/71 na kumtangaza mfalme wa Prussia kuwa Kaisari Wilhelm I wa Dola la Ujerumani.
- Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia washindi walikutana hapa na kuwa na mkutano kuhusu amani. Mkataba wa Versailles kuhusu amani na Ujerumani halafu mkataba wa Trianon kuhusu amani na Hungaria ilitiwa sahihi mjini.