Wikipedia:Makala kwa ufutaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta


Majadiliano ya awali yamehamishwa kwenye kurasa hizi:

Ongeza michango chini ya mstari wa mwisho!

Wikipedia:B56 Bplus CP

Haiwezi kubaki jinsi ilivyo (tazama: Majadiliano ya Wikipedia:B56 Bplus CP) kwa jina hilio pia nina wasiwasi kama ana umaarufu wowote. Labda Muddy aseme? Kipala (majadiliano) 13:32, 20 Juni 2014 (UTC)

Imehamishwa kwa ukurasa wa Cyprian Benedict Mwageni aliyeanza kuandika habari hizo kama ukurasa wake wa mtumiaji. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Sickora Gerald

Makala ilivyo haifai. Kwanza, imeandikwa na mhusika mwenyewe. Pili, siyo makala ya kamusi elezo bali ni sifa pamoja na uvutaji wa kununua muziki wake. Tatu, haijaonyeshwa kama mtu huyo angestahili kupata makala katika kamusi elezo, yaani, kama ni mtu mwenye umuhimu wa kutosha katika jamii ya Tanzania. Lazima kumwambia mwandishi ajieleze. La sivyo, makala na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:43, 29 Julai 2014 (UTC)

Kino

Makala ya Kiingereza; yaliyomo yalingana zaidi na wikikamusi. Kipala (majadiliano) 14:00, 7 Agosti 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Malick bandawe

Makala imeandikwa Kiingereza na haina viwango vya Kiwiki hata punje. Ninapendekeza ifutwe haraka iwezekanavyo!--MwanaharakatiLonga 13:47, 20 Agosti 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Sosholoji

Makala ilivyo haileti maana. Hata kichwa cha makala ni kosa. Mada huitwa "sosiolojia" au "elimujamii". Makala hii na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)