Uwanja wa michezo wa Nairobi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Nairobi ni uwanja wenye shughuli mbalimbali za kimichezo huko Nairobi nchini Kenya. Upo mashariki mwa jiji la Nairobi. Uwanja huo unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Nairobi.

Uwanja huo hapo awali ulijulikana kama Uwanja wa Afrika kisha ukapewa jina la Uwanja wa Barabara ya Donholm. Uwanja huo ulibadilishwa jina na kuitwa Uwanja wa Barabara ya Jogoo baada ya Kenya kupata uhuru mnamo mwaka 1963 na mwishowe ukaitwa Uwanja wa Jiji la Nairobi.

Ulikuwa uwanja mkuu jijini Nairobi hadi miaka ya 1980 wakati Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo na Moi International Sports Center vilijengwa. Uwanja huu unatumiwa zaidi kwa mechi za chama cha mpira wa miguu na ndio uwanja wa nyumbani wa Gor Mahia na vilabu vingine vya hapa. Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu takribani 15,000.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Nairobi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.