Ujain
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ujain au Jina Dharma ni dini yenye asili ya Kihindi na wafuasi wake huitwa Wajain. Ilianzishwa mnamo mwaka 500 KK. Kuna waumini milioni 6 duniani na zaidi ya nusu wako Uhindi.
Wajain hukumbukwa walimu 24 wa dini yao wanaoitwa "thirtankara". Thirtankar wa 24 alikuwa Mahavira wakati wa karne ya 6 KK anayetajwa mara nyingi kama mwanzilishaji wa dini ingawa wenyewe husema hakuna liyeanzisha hasa.
Kama Ubuddha ni dini isiyo na mafundisho kuhusu Mungu au miungu. Vilevile kama Ubuddha ilianzishwa katika mazingira ya Uhindu wa kale ikikataa tabaka za kidini jinsi ilivyo katika Uhindu.
Ujain inalenga kwa ukombozi wa nafsi ya mwanadamu. Kwa ukombozi huu ni muhimu mtu ajifunze kujitawala kwa sababu kila tenda linafuatwa na mazao yake yanayoitwa Karma. Nafsi katika imani ya Kijain huzaliwa tena na tena katika mwili mpya na shabaha ni kutozaliwa tena lakinimkupata ukombozi na starehe ya milele. Nafsi au roho hizi haziko ndani ya watu pekee lakini pia ndani ya wanyama.
Kila tendo linalosababisha mateso kwa kiumbe mwingine linarudisha nafsi katika mzunguko wa kuzaliwa tena. Matendo yanayoharibu karma ya mtu ni hasa mauaji ya viumbe wenye nafsi.
Kwa hiyo Ujain hufundisha kuepukana na uhasama na kutomtendea yeyote kwa mabavu. Kwa sbabu hii Wajain hukataa kula nyama kwa sababu nyama inapatikana kwa njia ya kuua na kutesa wanyama ambao no ni makazi ya nafsi sawa na wanadamu.
[hariri] Viungo vya Nje
| Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ujain kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
completed in