Ubuntu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Obuntu" ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Neno ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na KiXhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwaKiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Obuntu.
Falsafa ya obuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi. Msingi wa falsafa hii ni, "mtu sio mtu bila watu," kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu." kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu" Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya obuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na kidini kwakuwa imejengwa juu ya upendo wa watu wengine (kama unavyojipenda wewe) na hata mazingira.
Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu binafsi katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi.
[hariri] Viungo vya Nje
- Obuntu: Falsafa ya Kiafrika]tena ya kabila la kihaya katika Tanzania
- ubuntu: Falsafa ya Kiafrika Ubuntu na Sheria Afrika Kusini
- Bill Clinton Akisisitiza Kuhusu Ubuntu
- video
- Makala Kuhusu Ubuntu na Dini
- Tafsiri ya Ubuntu Toka Kwa Askofu Desmond Tutu
- Video: Mandela Akitafsiri Ubuntu
- Video ya Mandela Akizungumzia Ubuntu