Tume ya Mrosso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tume ya Mrosso (kwa Kiingereza: The Mrosso Commission; kifupi TMC) ilikuwa tume ya sheria nchini Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Iliundwa mwaka 1993 chini ya uelekezi wa Jaji Mkuu wa Tanzania Francis Nyalali. Tume ya Mrosso iliundwa ili kushughulikia changamoto za uendeshaji wa muda mrefu wa mahakama.

Ikiongozwa na Jaji John Mrosso, ilipendekeza hatua za kuboresha ufanisi wa mahakama, nidhamu na mahusiano ya umma. Tokeo mojawapo mashuhuri lilikuwa kuanzishwa kwa mfumo unaotambulika kama Utatuzi Mbadala wa Migogoro (ADR) katika kesi za madai kwenye mwaka 1994.

Tangu wakati huo njia ya ADR imekuwa sehemu muhimu ya mfumo wa sheria wa Tanzania na somo la lazima katika elimu ya sheria nchini. [1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Mkundi Legal. S, Alternative Dispute resolution (ADR) in Tanzania.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tume ya Mrosso kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.