Nenda kwa yaliyomo

Pepopunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tetanasi)
Mtu mwenye Pepopunda
Tetanasi
Mwainisho na taarifa za nje
ICD-10A33.-A35.
ICD-9037, 771.3
DiseasesDB2829
MedlinePlus000615
eMedicineemerg/574
MeSHD013742

Pepopunda, iitwayo pia Tetanasi (kutoka neno la Kiingereza lenye asili ya Kilatini: Tetanus), ni maambukizi yaliyo na sifa bainifu ya mvutano wa misuli. Katika aina ya kawaida sana mivutano huanza kwenye taya na kuenea kwenye sehemu nyingine za mwili. Mivutano hiyo kwa kawaida hudumu kwa muda wa dakika chache kila wakati na hutokea mara kwa mara kwa wiki tatu hadi nne.[1] Mivutano inaweza kuwa kali sana hata kuvunjika kwa mifupa kunaweza kutokea.[2]

Dalili nyingine zinaweza kujumuisha: joto jingi, maumivu ya kichwa, tatizo la kumeza, shinikizo la damu, na mpigo wa haraka wa moyo.[1][2]

Kuanza kwa dalili kwa kawaida huwa siku tatu hadi ishirini na moja baada ya maambukizi. Unaweza kuchukua miezi kabla ya kupona. Takribani asilimia 10 ya walioambukizwa hufariki dunia.[1]

Kisababishi na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Pepopunda husababishwa na maambukizi ya bakteria Kostridiamu tetani.[1] Kwa kawaida bakteria huingia mwilini kupitia mwanya kwenye ngozi kama vile mahali palipokatwa au jeraha lililosababishwa na kifaa chafu. Bakteria hizi hupatikana kwa kawaida kwenye udongo, vumbi na mbolea.[3] Bakteria hutoa toksini inayotatiza mikakamao ya misuli, huku ikisababisha dalili za kawaida.[4] Utambuzi huzingatia misingi ya ishara na dalili. Hugonjwa huu hauenei kati ya watu.[1]

Kinga, tiba na matarajio

[hariri | hariri chanzo]

Maambukizi yanaweza kuzuiwa kwa chanjo ya pepopunda.[5] Kwa wale walio na kidonda kubwa na chini ya dozi tatu za chanjo uchanjaji na globulini ya kinga dhidi ya pepopunda hupendekezwa. Kwa walioambukizwa globulini ya kinga dhidi ya pepopunda au iwapo haipatikani imunoglubolini ya kudunga mishipani (IVIG) hutumika. Kidonda kinapaswa kuoshwa na kila tishu iliyokufa kuondolewa.[1] dawa ya kulegeza misuli inaweza kutumika ili kudhibiti mivutano. Tundu lililoandaliwa la kupitisha hewa linaweza kuhitajika iwapo kupumua kwa mtu kumeathirika.[4]

Epidemiolojia na historia

[hariri | hariri chanzo]

Pepopunda hutokea katika sehemu zote za dunia lakini hutokea mara nyingi zaidi katika hali ya anga iliyo joto na iliyo na unyevunyevu pale ambapo udongo huwa na viumbe hai.[1] Katika mwaka wa 2013 ilisababisha takribani vifo 59,000 – idadi iliyopungua kutoka 356,000 katika mwaka wa 1990.[6] Maelezo ya ugonjwa huu na Hippocrates yamekuwa kutoka angalau karne ya 5 BCE. Kisababishi cha ugonjwa kiligunduliwa katika mwaka wa 1884 huku chanjo ikianzishwa katika mwaka wa 1924.[1]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Atkinson, William (Mei 2012). Tetanus Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (tol. la 12). Public Health Foundation. ku. 291–300. ISBN 9780983263135. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Tetanus Symptoms and Complications". cdc.gov. Januari 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Tetanus Causes and Transmission". www.cdc.gov. Januari 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Tetanus For Clinicians". cdc.gov. Januari 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. https://www.lifesitenews.com/news/new-documentary-exposes-world-health-organizations-vaccine-sterilization-campaign-in-kenya/
  6. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pepopunda kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.